Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na majasusi, ni kwamba balozi za Marekani na Uingereza zipo hatarini kushambuliwa miaka kadhaa baadaye. Siku ambayo ilipangwa kwa muda mrefu, kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani angetembelea ubalozi wa nchi yake jijini Dar es salaam.
Mashirika ya kijasusi ya nchi hizo yanaingiwa na mashaka makubwa, kutokana na habari walizopata bomu ambalo lingetumika kulipua lingetikisa jiji zima. Ndiyo hapo sasa inabidi EASA waingilie kati suala, na inakuja kubainika chimbuko la lote ni nchini Somalia.
Majasusi watatu wanatumwa huko, akiwemo Norbert Kaila wanafanya kazi yao vyema. Shida inakuja ni pale wakitaka kuondoka, na hapo mmojawapo alishagunduliwa kuwahi kufika nchini humo hasa jimbo la Juba akafanya maafa ambayo yalipelekea awekewe kisasi.
Inageuka kuwa operesheni ambayo ilikaribia kugharimu maisha yake, ili kufanikisha wenzake wengine watoroke na mtuhumiwa waliyekuwa wakimsaka hasa.